Kwa mujibu wa kundi la Tafsiri la Shirika la Habari la Hawza, Hojjat-ul-Islam wal-Muslimin Arif Hussein Wahedi, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Mshikamano la Kitaifa la Pakistan, katika kujibu matukio ya hivi karibuni ya Ghaza, kwa kulaani vitendo vya kikatili vya utawala haram wa Kizayuni na uungaji mkono wa Marekani, alisisitiza kwamba wananchi wa Palestina waliharibu mipango yote ya wavamizi wa Ghaza na kuitokomeza mitizamo yao dhidi ya Ghaza kwa kusimama imara, kupigana Jihad na imani.
Huku akiashiria juu ya ukatili wa kikatili na usio na kifani ambao waliutekelezwa dhidi ya watu wa Ghaza katika kipindi cha miezi kumi na tano iliyopita, amesema katika taarifa hii: Utawala wa Kizayuni haukuacha jinai zozote katika kipindi hiki.
Mashambulio ya kikatili ya mabomu, mzingiro wa kikatili, mauaji ya kikatili ya wanawake na watoto, uharibifu wa kushambulia na kubomoa hospitali na miundombinu, yote hayo yanaonyesha hali ya jinai ya utawala huu, lakini pamoja na ukatili huu wote, watu wa Ghaza bado hawakukata tamaa, bali kwa ujasiri, bidii na imani thabiti, walimshinda adui na kuonyesha kwa mara nyingine tena kwamba upinzani (Muqawamah) ndiyo njia pekee ya ushindi.
Your Comment